Swahili Hymn N-Z

Naendea msalaba


1. Naendea msalaba, Ni mnyonge, mpofu,
Yapitayo naacha nipe msalaba tu.


Ref
Nakutumaini tu, wee Mwana wa Mungu;
Nainamia kwako; Niponye sasa, Bwana.


2. Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi;
Pole Yesu asema: “Nitazifuta zote.”


3. Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
Roho yangu na mwili viwe vyako milele.


4. Kwa damu yake sasa amenivuta sana,
Upendo hubidisha, nimtafute Mwokozi.


5.Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake,
Kila chembe kamili; Msifuni yeye mponya!

 


Nasifu Shani Ya Mungu


Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua, nyota, mwezi,
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo,
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.


Kadiri ya nionayo, ya kusifu Mungu;
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu;
Hakuna hata unyasi, usiokukuza;
Na upepo wavumisha, au kutuliza.


Nami kwa mkoni wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupo, kukwomba ni dawa;
Umenizingira nyuma, na mbele baraka;
Maarifa ya ajabu! Yanishinda mimi!

 


Nasikia Sauti Yako


1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.


Refrain
Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.


2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.


3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.


4. Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.

 


Neema ya Ajabu


1. Neema ya upendo wake
Neema kuu liko nami;
Kazi ya Yesu msalabani
Alipo mwaga damu yake.


Refrain
Neema yake, Neema, ya ajabu
Neema inayotakasa;
Neema yake, Neema, ya ajabu
Neema ishindayo dhambi.


2. Dhambi ni kama wimbi kubwa
Inayotishia maisha;
Ni neema isiyo kifani
Inayo ‘nyesha msalabani.


3. Neema hii ni ya ajabu
Iliyo bure kwetu sisi;
Wanaotaka kumuona
Watapata neema ya bure.