Swahili Hymn N-Z

Siku Kuu


1. Ni siku kuu, siku ile, ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele, kunyamaza hauwezi.


Refrain
Siku kuu! siku kuu! ya kuoshwa dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu, ananiongoza miguu
Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.


2. Tumekwisha kupatana, mimi mbwake, yeye mbwangu;
Na sasa nitamwandama, nakiri neno la Mungu.


3. Moyo tulia kwa Bwana, kiini cha raha yako;
Huna njia mbili tena; uwe naye, yote ndako.

https://youtu.be/dsxyrMnjwHo

 


Siku ya Mbingu Kujawa Na Sifa


Siku ya Mbinguni kujawa na sifa,
Dhambi zilizidi duniani;
Yesu akaja azaliwe mtu,
Awe na watu ulimwenguni.


Ref
Alinipenda, alinifia,
Ameondoa na dhambi zangu;
Alifufuka nipewe haki,
Yuaja tena Mwokozi wangu.


Na siku moja walikwenda naye,
Wakamkaza msalabani;
Aliumia, aliaibishwa,
Ili atuokoe dhambini.


Siku hiyo wakamlaza chini
Kaburini alipumzika;
Matumaini yetu wenye dhambi,
Ni mwokozi, kwake twaokoka.


Kaburi likashindwa kumshika;
Jiwe likatoka mlangoni,
Alifufuka kwa kushinda kwake,
Naye yuko milele Mbinguni.


Siku moja atatujia tena;
Utukufu wake tutaona;
Atawaleta na wapenzi wetu;
Mwokozi: wangu, tutaonana.

 


Sioshwi Dhambi Zangu


Sioshwi dhambi zangu,
Bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu,
Bila damu yake Yesu.


Refrain
Hakuna kabisa,
Dawa ya makosa,
Ya kututakasa,
Ila damu yake Yesu.


La kunisafi sina,
Ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena,
Ila damu yake Yesu.


Sipati patanishwa,
Bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha,
Bila damu yake Yesu.


Sipati tumaini,
Bila damu yake Yesu,
Wema wala amani,
Bila damu yake Yesu.


Yashinda ulimwengu,
Hiyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu,
Hiyo damu yake Yesu.


Twaimba utukufu,
Una damu yake Yesu,
Milele twaisifu,
Hiyo damu yake Yesu.