Swahili Hymn N-Z

Nilitembea mbali katika dhambini


Nilitembea mbali katika dhambini,
Nikapoteza hali nikashuka chini;
Kwake Mwokozi Bwana, nikamlilia
Akanishika sana kuokoa.


Ref
Na upendo, Na upendo,
Nimeinuliwa sana na upendo;
Na upendo, Na upendo,
Nimeinuliwa sana na upendo;


Moyo wangu nampa, nitamshika pia
Nitakaa na Yesu, sifa kumwimbia:
Upendo wa hakika wastahili sifa,
Na uaminifu ni wake pia.


Mliomo shidani, tazameni Bwana,
Atawaponya kweli, kutoka mashaka;
Atawasimamisha na upendo wake,
Awe Mwokozi kwa wokovu wake.

 


Nimekombolewa na Yesu


Nimekombolewa na Yesu
Aliyenirehemia;
Kwa bei ya mauti yake
Nimekuwa mtoto wake.


Ref
Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.


Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Nimekuwa mtoto wake.


Nitamwona uzuri wake,
Mfalme wangu wa ajabu;
Na sasa najifurahisha,
Katika neema yake.


Najua taji imewekwa
Mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
Ili alipo, niwepo.

 


Nimshangilie Bwana wangu