Swahili Hymn N-Z

Nipe Habari Za Yesu


1. Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana:
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sasa.
Jinsi malaika wengi walivyo imba sifa,
Alipoleta amani kwa watu wa dunia.


Ref
Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha thamani Hunipendeza sana.


2. Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani.
Jinsi alivyomshinda Jaribu la Shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni ya ajabu!


3. Habari za Msalaba Alivyosulubiwa;
Jinsi walivyo mzika, Akashinda kaburi.
Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu.
Aliyetoa maisha Nipokee wokovu.

 


Nitamshukuru Mungu


Nitamshukuru Mungu,
Kwa upendo wake mkuu,
Alimtuma Mwanawe,
Kunifilia mimi.


Ref
Kweli nitaimba nyimbo,
Za upendo wake mkuu,
Pamoja na malaika,
Walioko mbinguni


Nalifanya dhambi nyingi,
Nilikaa maovuni,
Bali nimeokolewa,
Yesu hunisafisha.


Amenipa Roho yake,
Anijaze daima,
Nimekuwa mwana wake,
Hunipenda kabisa.


Mungu wangu, nashukuru
Husujudu daima,
Neno lako nitangaze,
Kwa upendo popote.

 


Nitaonana na Yesu


1. Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli,
Siku ile shangwe tele, nikimwona Mwokozi.


Kiitikio:
Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni, Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.


2. Sasa siwezi kujua, jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.


3. Mbele yake yafukuzwa, machozi na huzuni,
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.


4. Uso kwa uso hakika, pale pale furaha,
Nitafurahi kabisa, nikimwona Mwokozi.