Ati Kuna Mvua Njema
1. Ati, kuna mvua njema yanya yenye neema;
Watu wanaona vyema Bwana, huninyeshei?
Refrain
Na mimi? Na mimi? Bwana, huninyeshei?
2. Sinipite, Baba Mwema; dhambini nimezama;
Rehema niza daima; Bwana hunionyeshi?
3. Sinipite, Yesu Mwema; niwe nawe daima,
Natamani kukwandama: Bwana, hunichukui?
4. Sinipite, Roho Mwema, Mpaji wa uzima,
Nawe shahidi wa wema, Bwana wema hunipi?
https://youtu.be/2079l5QnXtw
Baba Yetu Aliye Mbinguni
Baba yetu aliye mbinguni, Amenifurahisha yakini;
Kuniambia mwake Chuoni, Ya kuwa nami Yesu pendoni.
Refrain:
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, Anipenda:
Anipenda, Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.
Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli:
Hunirejeza kwake moyoni, Kweli yu nami Yesu pendoni.
Anipenda! Nami ninampenda, Kwa wokovu alionitenda;
Akanifilia Msalabani, Kwa kuwa nami Yesu pendoni.
https://youtu.be/MdsTqoGAWh0
Bwana upepo wavuma
Bwana upepo wavuma! Wimbi lina ghadhabu! Wingu hili linanguruma bandari si karibu,
Hali yetu hufikiri kwa nini kulala? Twafa maji yawe ni karibu wokovu la! Hapana
Refrain
Pepo na mawimbi vyasikia tulia, tulia, kama ukali wa bahari, wanadamu, pepo na shetani
Mawimbi yapataje kuumiza chombo kilicho na Yesu Bwana?
Mambo pia viamsikia tulia, tulia Mambo pia viamsikia tulia, tulia
Bwana nimezima moyo hamu yanizidi tu ninasumbuka roho yangu uniokoe Bwana;
Dhambi nyingi na uovu zitanizamisha Bwana wangu upesi ni wewe utakaenitosha,
Sasa hofu imekwisha ni shwari baharini, Jua letu tena linang’ara utulivu rohoni
Kaa nami ewe Bwana nisiwe mimi tu nami nitafika bandarini ng’ambo niko nafuu