Mwokozi ajabu ni Yesu bwana
https://youtu.be/KsFTSvGUMYs
Mwokozi kama mchunga
Mwokozi kama mchunga
Utuongoze leo;
Ututume malishoni;
Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako
Umetuvuta kwako.
Tu wako, uwe rafiki,
Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde,
Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu tusikie,
Tukiomba, samehe.
Umetuahidi kwamba
Utakubali watu,
Utawahurumia na
Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda
Kuwa wako.
Mwokozi niongozwe
Mwokozi Niogoze Nisipotee kamwe,
Nina salama kwako, Nikae nawe pako
Ref
Yesu, Yesu, Niogoze nisipotee,
Maisha yamgu yote, Mwokozi unishike.
Eh, kimbilio langu, Wakati dhuruba kuu,
Nina salama yako, Kutegemea kwako.
Mwokozi unishike, Hata nichukuliwe;
Mpaka nchi ya mwanga, Mle chozi hapana.
Mwokozi wangu umekosa nini
Mwokozi wangu, umekosa nini?
Wahukumiwa kama mwuaji.
Umeshtakiwa makosa
Uliyotenda?
Wapigwa sana, miiba taji lako,
Umetemewa mate, watukanwa,
wanyweshwa nyongo,tena siki kali,
Wasulibishwa!
Sababu gani unateswa hivi?
Makosa yangu yanakuumiza;
Mateso haya yako yanipasa,
Mimi mkosaji.
Ajabu kubwa sana tendo lako:
Mchungaji unateswa kwa ajili
Ya kondoo, Bwana unawalipia
Watumwa wako.
Tulipokuwa mateka ya mwovu,
Nawe ukaja ukatukomboa.
Twalistahili kufa kwa milele,
Ukatufia.
Mwokozi wangu nifanyeje mimi,
Niitangaze pote sifa yako?
Nakufuata nikutumikie
Maisha yote.