Swahili Hymn A-M

Lo Ajabu Kupata Uzima


Lo! Ajabu kupata Uzima, katika damu ya Mwokozi wangu!
Alinifilia pendoni, Mimi niliyemsulubisha!
Upendo huu wa kushangaza kabisa Wewe Kristo wangu kunifilia pendoni
Upendo huu nashangaa Kristo wangu kunifilia


wangu alitoa damu Siwezi kuelewa neno hili,
Viumbe vyote vya mbinguni Navyo haviwezi kufahamu
Najua tu ni kwa rehema zake Mungu Malaika wote wamsujudu Mungu
Ni rehema tumwabudu, Tumwamini ndiye mwokozi


Aliondoka kule mbinguni Kwa nyumba yake Mungu Baba yake
Na utukufu aliacha Afe kwa ajili ya waovu
Rehema zake ni nyingi na ukarimu Kwani Mungu wangu aliniokoa mimi
Sistahili neema yake, Lakini aliniokoa


Roho yangu ilifungwa sana Dhambi na giza vilinilemea
Ukaniangaza rohoni, Gereza yangu ikaang’aa mno
Ikafunguka minyororo yangu yote Nikaondoka nikaanza kukufuata
Siku ile nitapata Uhuru kweli kwako Mungu


Hukumuni mimi simo sasa Mimi ni wake Yesu ndiye wangu
Yeye ni kichwa changu kweli Na amenivika haki yake
Mimi hodari sasa kwa kiti cha Enzi Napewa taji ya milele katika Yesu
Sina hofu kusogea Katika Bwana wangu Kristo

 


Malaika kaleta noeli


Malaika kaleta Noeli ya kwanza,
Kwa wachunga kondoo katika makonde,
Bethlehemu wakawa walinzi wa zamu,
Wakaona usiku ajabu ya nuru


Refrain
Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu
Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu


Wakaona mbinguni, mwangaza wa nyota,
Ing’aayo kwa mbali na masharikini,
Wakaenda upesi, walivyoambiwa.
Bethlehemu wamwone Mwokozi horini


Mashariki watoka wafalme watatu,
Mamajusi waliotafuta mfalme,
Wafuata hii nyota waliyoiona,
Wasipate kumkosa wanayemtafuta


Kiongozi ni nyota iliyowaleta
Hata mji wa Daudi alimozaliwa
Ikakaa mara moja isiendelee
Pale pale nyumbani alimo Mwokozi


Mamajusi walipoingia nyumbani
Wakapiga magoti kwa heshima kuu
Mara hiyo walipozifungua hazina
Manemane, uvumba, dhahabu, watoa

 


Mapenzi yako yafanyike


Mapenzi yako yafanyike,
Wewe mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.


Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji dhambi zote,
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.


Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.


Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote,
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.


Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike,
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.


Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote,
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho nayo nguvu.