Swahili Hymn A-M

Kaa Nami


1. Kaa nami ni usiku tena; usiniache gizani, Bwana,
Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.


2. Siku zetu hazikawi kwisha; Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.


3. Nina haja nawe kila saa; sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani ila wewe? Bwana kaa nami.


4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviniumi; Nitashinda kwako, kaa nami.


5. Nilalapo nikuone wewe; Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote; kaa nami.

https://youtu.be/MB03jkJ5q_0

 


Karibu na wewe


Karibu na wewe, Mungu wangu: Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.


Mimi nasafiri duniani, Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.


Yote unipayo yanivuta; Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.


Na kwa nguvu zangu nikusifu; Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe; Karibu zaidi, Mungu wangu.


Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.

 


Kumtegemea Mwokozi


1. Kumtegemea Mwokozi, Kwangu tamu kabisa;
Kukubali neon lake nina raha moyoni


Chorus
Yesu, Yesu namwamini, nimemwona thabiti;
Yesu, Yesu yu thamani, ahadi zake kweli.


2. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kuamini damuyake nimeoshwa kamili


3. Kumtegemea Mwokozi, kwangu tamu kabisa;
Kwake daima Napata, uzima na amani.


4. Nafurahi kwa sababu, nimekutegemea;
Yesu, M-pendwa, Rafiki, uwe name dawamu