Nina haja Nawe
Nina haja nawe
Kila saa;
Hawezi mwingine
Kunifaa.
Refrain
Yesu nakuhitaji
Vivyo kila saa!
Niwezeshe Mwokozi,
Nakujia.
Nina haja nawe;
Kaa nami,
Na maonjo haya,
Hayaumi.
Nina haja nawe;
Kila hali,
Maisha ni bure,
Uli mbali.
Nina haja nawe;
Nifundishe
Na ahadi zako
Zifikishe.
Nina haja nawe;
Mweza yote,
Ni wako kabisa
Siku zote.
Ninao wimbo mzuri
1. Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa Mkombozo Mfalme, Tangu kuamini.
Refrain:
Tangu kuamini, Tangu kuamini, Jina lake ‘tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu jina lake.
2. Kristo anatosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.
3. Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.
4. Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.
Niongoze, Bwana Mungu
1. Niongoze, Bwana Mungu, Ni msafiri chini;
Ni mnyonge, nguvu Sina; Nishike mkononi,
U mkate wa Mbinguni, Nilishe siku zote
Nilishe siku zote
2. Kijito cha maji mema, Kitokacho mwambani,
Nguzo yako, moto,wingu Yaongoza jangwani;
Niokoe Mwenye nguvu; Nguvu zangu na ngao
Nguvu zangu na ngao
3. Nikikaribia kufa, Sichi neno lo lote
Wewe kifo umeshinda Zinawe nguvu zote.
Tutaimba sifa zako, Kwako juu milele
Kwako juu milele