Swahili Hymn N-Z

Nasikia Sauti Yako


1. Nasikia mwito, Ni sauti yako;
Nikasafiwe kwa damu Ya kwangikwa kwako.


Refrain
Nimesongea mtini pako,
Unisafi kwa damu ya kwangikwa kwako.


2. Ni mnyonge kweli, umenipa nguvu;
Ulivyonisfi taka Ni utimilivu.


3. Yesu hunijuvya: Mapenzi imani,
Tumai, amani, rahi, hapa na mbinguni.


4. Napata wokovu, Wema na neema;
Kwako Bwana nina nguvu Na haki daima.

https://youtu.be/CaXmhRjh09U

 


Nataka Nimjue Yesu


Nataka nimjue Yesu
Na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili


Refrain:
Zaidi, zaidi
Nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili


Nataka nione Yesu
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni
Kujidhihirisha kwangu


Nataka nifahamu
Na nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye
Yale yanayompendeza


Nataka nikae naye
Kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake

 


Ndiyo dhamana


Ndiyo dhamana, Yesu wangu,
Hunipa furaha za mbingu,
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa roho wake.


Ref
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.


Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu,
Aniletea malaika,
Wanilinda, taokoka.


Sina kinyume; nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu,
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu; ndimi nuru.


Hali na mali, anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangonja kwa subira,
Akiniita nije mara.