Nataka kusimama
Nataka kusimama, chini ya msalaba.
Kama kivuli cha mwamba, wakati wa mchana.
Kama ni maji nyikani, kambi safarini.
Na hapa nitapumzika, kwani jua kali.
Mahali pema sana, chini ya msalaba.
Kwani hapo ninaona, upendo wa Yesu.
Yakobo alivyoona, ndotoni zamani.
Mti Yesu aliowambwa, ni ngazi kwa Mungu.
Juu ya msalaba huo, Yesu alikufa.
Alikufa tuokoke, tuliopotea.
Ninastaajabu kabisa, Ni mambo mawili;
Kwake Yesu ni upendo, kwangu mimi kosa!
Wataka kuonana, na Yesu mbinguni,
Yakupasa kukaa kwanza, chini ya mti huo.
Ni kweli siku chache tu, mateso na shaka.
Halafu pasipo mwisho, furaha kwa Bwana!
Nataka Nimjue Yesu
Nataka nimjue Yesu
Na nizidi kumfahamu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili
Refrain:
Zaidi, zaidi
Nimfahamu Yesu
Nijue pendo lake na
Wokovu wake kamili
Nataka nione Yesu
Na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni
Kujidhihirisha kwangu
Nataka nifahamu
Na nizidi kupambanua
Mapenzi yake nifanye
Yale yanayompendeza
Nataka nikae naye
Kwa mazungumzo zaidi
Nizidi kuwaonyesha
Wengine wokovu wake
Nchi nzuri yametameta
Nchi nzuri yametameta,
Huonekana kule mbali;
Naye Yesu hutuongoza,
Tukafike na sisi huko.
Refrain
Si mbali, karibu,
Tutaimba na sisi huko!;
Si mbali, karibu,
Tutaimba na sisi huko!
Kule tutawaona wengi,
Wapendwao na Yesu Bwana,
Tutashirikiana nao,
Itakuwa furaha kubwa,
Tutamwona na Bwana wetu,
Yesu Kristo Mwokozi wetu.
Tutashangilia daima,
Tuna hamu ya kwenda kwetu.
Ndiyo dhamana
Ndiyo dhamana, Yesu wangu,
Hunipa furaha za mbingu,
Mrithi wa wokovu wake,
Nimezawa kwa roho wake.
Ref
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu,
Habari njema, raha yangu,
Yesu ndiye Mwokozi wangu.
Kumsalimu moyo wangu,
Mara namwona raha yangu,
Aniletea malaika,
Wanilinda, taokoka.
Sina kinyume; nashukuru,
Mchana kutwa huja kwangu,
Usiku kucha kuna nuru,
Mwokozi wangu; ndimi nuru.
Hali na mali, anitwaa!
Mara namwona anifaa,
Nami nangonja kwa subira,
Akiniita nije mara.