Nitembee Nawe
Nitembee nawe Mungu, Alivyotembea Henok;
Mkono wangu uushike; Unene nami kwa upole;
Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe.
Siwezi tembea pekee; Pana dhoruba njiani;
Mitego ya miguu elfu; Adui wengi hufichwa;
Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe.
Ukinishika mkono Anasa kwangu hasara;
Kwa nguvu nitasafiri; “Tautwika msalaba;
Hata mji wa Zayuni Yesu nitembee nawe.
https://youtu.be/pENcA_z-If4
Nitwae hivi nilivyo
Nitwae hivi nilivyo,
Umemwaga damu yako,
Nawe ulivyoniita,
Bwana Yesu, naja, naja.
Hivi nilivyo si langu,
Kujiosha roho yangu,
Nisamehe dhambi zangu,
Bwana Yesu, naja, naja.
Hivi nilivyo sioni,
Kamwe furaha moyoni,
Daima ni mashakani,
Bwana Yesu, naja, naja.
Hivi nilivyo kipofu,
maskini na mpungufu,
Wewe u mtimilifu,
Bwana Yesu, naja, naja.
Nawe hivi utanitwaa;
Nisithubutu kukawa,
Na wewe hutanikataa,
Bwana Yesu, naja, naja.
Hivi nilivyo mapenzi,
Yamenipa njia wazi,
Hali na mali sisazi,
Bwana Yesu, naja, naja.
Njia yote naongozwa
1. Njia yote naongozwa kwa mukono wa Mwokozi;
Ninaona wema wake, sina shaka wala woga,
Nina raha ya mbinguni, na salama tamu sana,
Na katika mambo yote ananitendea mema.
Na katika mambo yote ananitendea mema.
2. Njia yote naongozwa, ninategemea Yesu;
Anilinda jaribuni, ananipatisha nguvu.
Nikiona kiu hapa, nikichoka kwa safari,
Ninapata maji mengi toka Mwamba wa milele.
Ninapata maji mengi toka Mwamba wa milele.
3. Njia yote naongozwa kwa mapendo yake bora;
Ananituliza sana na ahadi yake nzuri.
Nitafika kwake mbingu kufurahi kwa milele,
Nitaimba neno hili, Yesu aliniongoza.
Nitaimba neno hili, Yesu aliniongoza.
Njooni Tuimbe Wimbo Huu
Njooni tuimbe wimbo Huu:
Atupenda!
Mungu ni mwenye huruma!
Atupenda!
Miolala amkeni, Mumtafufuteni mwokozi!
Woga na kufa uishe!
Atupenda!
Ref
Atupenda! Atupenda!
Njooni tuimbe wimbo huu: Atupenda!
Utume mwema ndio Huu:
Atupenda!
Alitujia toka juu,
Atupenda!
Mwanawe Mungu, Mwokozi Atuita sote;
Njooni! Mlioshindwa na mwovu.
Atupenda!
Ametufia Golgota,
Atupenda!
Katupatia uzima,
Atupenda!
Mponya ni jua la watu. Yeye ni ngao vitani.
Tumtafuteni kwa bidii,
Atupenda!
Maharbuni atufaa,
Atupenda!
Atukaribisha kwake,
Atupenda!
Yeye ni mfalme na shujaa. Yeye hachoki kulinda!
Watu wote wamwombao,
Atupenda!
Njooni tumsifuni Mungu
Njooni tumsifuni Mungu Aliye Mwenyezi.
Mfalme wa popote Mbinguni na duniani.
Kwa sauti kuu Wote wamsifu Mungu,
Kumpigia Mfalme shangwe.
Njooni tumsifuni Mungu Anayetawala
Vyote vizuri Akuongozaye na wewe.
Waruka juu Kama kwa nguvu ya tai.
Ukiongozwa na Mungu.
Njooni tumsifuni Mungu Aliyetuumba
Aliyetupa uzima Na wingi wa neema.
Shida nyingi Zimefukuzwa kwetu
Na Mungu mwenye rehema.
Njooni tumsifuni Mungu Aliyetulinda.
Atubariki kwa pendo, Atupa riziki.
Ni Mwenyezi, Atutendea makuu
Anatupenda kwa kweli.
Njooni tumsifuni Mungu Tumsifu kwa nyimbo,
Kama Daudi imbeni na Mashangilio
Tusisahau ndiye nuru ya roho.
Tumsifu hata milele.