Amani moyoni
Tangu siku hiyo aliponijia,Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia, Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Ref
Amani moyoni mwangu, Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe Kwa sababu yeye. Yu nami moyoni mwangu.
Sina haja tena ya kutanga-tanga, Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu Mwanawe Mungu.
Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka, Kwa kuwa ninaye Yesu.
Siogopi tena nikiitwa kufa, Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi, ’Tapita humo kwa damu.
Nitaketi na Yesu huko milele, Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu Mwanawe Mungu.
Amini Jina La Yesu
Amini Jina La Yesu, wewe upoteaye,
Utafurahishiwa nalo, liamini kwa kweli.
Ref
Jina la Mwokozi, furaha ya mbimguni,
Jina la Mwokozi, tumaini la watu.
Tembea na jina hili, la Yesu siku zote,
Ndiyo ngome jaribuni, uwezo maombini.
Jina lake Yesu Kristo, tunalifurahia,
Kwa maana alikuja, tuipate amani.
Jina lake Yesu Kristo, tutalisujudia,
Mfalme wa wafalme wote, tutamsifu mbinguni.
Amini utii
Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.
Ref
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii
Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa,
Woga, wasiwasi, sononeko, basi.
Huamini nitii pia.
Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia,
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki,
Taamini nitii pia.
Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.
Nitamfurahisha na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia