Ni siku ya furaha
1. Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru;
Nasi twaona raha, Kuja kushukuru;
Leo watu wa Mungu, wadogo, wakubwa,
Hukaribia mbingu, lilipo baraka.
2. Leo, ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili:
Kijito cha baridi kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.
3. Leo ngazi na iwe ifakayo juu,
Mawazo na yasiwe ya duniani tu;
Leo ni kujilisha chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha kwa mambo ya Mungu.
Ni Tabibu wa Karibu
1. Ni tabibu wa karibu, Tabibu wa ajabu,
Na rehema za daima, Ni dawa yake njema.
Ref
Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana
Pweke limetukuka, Jina lake Yesu.
2. Hatufai kuwa hai, wala atutumai,
Ila yeye kweli ndiye Atupumzishae.
3. Dhambi pia na hatia, Ametuchukulia
Twenendeni kwa Amani, Hata kwake Mbinguni.
4. Huliona tamu jina, La yesu kristo bwana,
Yuna sifa mwenye kufa, Asishindwe na kufa.
5. Kila mume asimame Sifa zake zivume;
Wanawake na washike, Kusifu jina lake.
6. Na vijana vyote tena, Vimpendavyo sana;
Vije kwake viwe vyake, Kwa utumishi wake.
Ni wako Bwana
1. Ni wako Bwana, ninasikia Unaponena nami;
Lakini, kweli, nataka kwako Nizidi kusongea.
Refrain
Bwana vuta, (vuta) nije nisongee
Sana kwako mtini.
Bwana, vuta, vuta, nije nisongee
Pa damu ya thamani.
2. Niweke sasa nikatumike kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende Nizidi kukwandama.
3. Nina furaha tele kila saa nizungumzapo nawe;
Ninanena kama kwa rafiki Nikipiga magoti.