Swahili Hymn N-Z

Neema ya pekee


Katika neema Nimeokolewa, Nilikuwa mimi Mnyonge
Nilikuwa kipofu bali neema ya Yesu, ilinifungua macho yangu


Nilikuwa mwenye hofu nilifungwa dhambini, nimefunguliwa sasa
Nitamsifu Bwana maishani mwote, kwani nina ushirika naye


Bwana ameniahidi mema, neno lake tumaini laokoa
Yeye atakuwa ngao yangu, siku zote maishani mwangu

 


Ni Heri Kifungo


Ni heri kifungo, Kinachotufunga
Mioyo yetu kwa pendo, Pendo la Kikristo


M-bele ya Baba Tunatoa sala;
Hofu, nia, masumbufu Yetu ni pamoja.


Tunavishiriki Matata na shida;
Na mara nyingi twatoa Chozi la fanaka.


Tunapoachana, Moyoni twalia;
Lakini tutakutana M-wisho mbinguni.

https://youtu.be/ZzR2n9weWq4

 


Ni salama rohoni mwangu


Nionapo amani kama shwari,
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha,
Ni salama rohoni mwangu.


Refrain
Salama, Salama,
Rohoni, Rohoni,
Ni salama rohoni mwangu.


Ingawa Shetani atanitesa,
Nitajipa moyo kwani;
Kristo ameona unyonge mwangu,
Amekufa kwa roho yangu.


Dhambi zangu zote, wala si nusu,
huwekwa Msalabani;
Wala sichukui laana yake,
Ni salama rohoni mwangu.


Ee Bwana himiza siku ya kuja,
Panda itakapolia;Utakaposhuka sitaogopa,
Ni salama rohoni mwangu.