Swahili Hymn N-Z

Yesu nakupenda, U mali yangu


1. Yesu nakupenda, U mali yangu,
Anasa za dhambi sitaki kwangu;
Na Mwokozi aliyeniokoa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.


2. Moyo umejaa mapenzi tele
Kwa vile ulivyonipenda mbele,
Uhai wako ukanitolea
Sasa nakupenda, kuzidi pia.


3. Ulipoangikwa Msalabani
Tusamehewe tulio dhambini;
Taji ya miiba uliyoivaa,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.


4. Niwapo hai, niwapo maiti,
Kupendana nawe kamwe siachi;
Hari za kifo zikinienea,
Sasa nakupenda, kuzidi pia.


5. Mawanda mazuri, na masikani
Niyatazamapo huko Mbinguni,
Tasema na taji nitakayovaa
Sasa nakupenda, kuzidi pia.

 


Yesu ni Jina Nipendalo


Yesu ni jina nipendalo. Napenda kulisikia;
Napenda kulitamka hilo, Lililoniridhisha.


Chorus
Yesu, nakupenda, Yesu, nakupenda;
Yesu, naktipenda, Kwani ulinipenda.


Jina hilo huniambia, Mwokozi alinipenda;v Damu yake ilimwagika, Nipate kuokoka.


Lanionyesha sifa yake, Iliyo katika Baba;
Njia ijapokuwa giza, Yesu huniongoza.


Lanidhihirishia Yesu, Aliyenihurumia;
Laondoa taabu yangu, Niwe wake daima.

 


Yote namtolea Yesu


Yote namtolea Yesu, Nampa moyo wote,
Nitampenda siku zote, Namwandama kila saa.


Chorus
Yote kwa Yesu,Yote kwa Yesu,
Yote kwako, Ee Mwokozi, Natoa sasa.


Yote namtolea Yesu, Nainamia pake;
Nimeacha na anasa, Kwako Yesu nipokee,


Yote namtolea Yesu, Nifanye niwe wako;
Nipe Roho yako, Bwana, Anilinde daima,


Yote namtolea Yesu, Nami naona sasa;
Furaha ya ukombozi, Nasifu jina lake.