Swahili Hymn N-Z

Njooni Tumuabudu


1. Njoni na furaha, Enyi wa Imani,
Njoni Bethlehemu upesi!
Amezaliwa mjumbe wa Mbinguni


Ref
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.


2. Jeshi la mbinguni, Imbeni kwa nguvu!
Mbingu zote na zijae sifa!
Sifuni Mungu aliye mbinguni;


3. Ewe Bwana Mwema, Twakubarikia,
Yesu, utukufu uwe wako;
Neno la Baba limekuwa mwili;

 


Nmeitaji Mwokozi


1. Nimehitaji Mwokozi
Awe nami daima;v Nataka mikono yake,
Kunizunguka sana.


Ref
Hofu rohoni sina,
Aniongoza tena;
Sitanung’unika tena,v Nimfuate daima.


2. Nimehitaji Mwokozi,
Sina imani nyingi;
Atanifufusha moyo,v Wengine hawawezi.


3. Nimehitaji Mwokozi,
Mwendoni mwa maisha;
Katika mateso mengi,v Tena katika vita.


4. Nimehitaji Mwokozi,
Kiongozi njiani;
Kwa jicho aniongoze,v Ni’fike mbinguni.

 


Nuru Ya Mbingu


1. Uwe nuruni kwenye safarini kwenye milima na mabonde
Yesu anasema hata tuache usimwache akusihi.


Chorus
Nuru ya mbingu Nuru ya mbingu utukufu umefurika
Alleluia Ninafurahi nitamwimbia Yesu wangu.


2. Nimezungukwa na giza nene sikumtambua Mwokozi
Yeye ni nuru hakuna giza nitatembea naye Bwana.


3. Nafurahia nuru ya Yesu makao yameandaliwa
Naimba sifa zake Mwokozi natembea nuruni mwake.

https://youtu.be/c6oiT5pOLbA