Swahili Hymn N-Z

Usiku Mtakatifu


Usiku mtakatifu, nyota zameremermeta
Ni usiku wa kuzawa mwokozi
Dunia yote, kwa dhambi ilizama
Hadi Yesu kaja kutuokoa
Tunaiingia ya kusisimua kote
Utukufu wake wachomoza
Tumsujudu, sikia malaika
Usiku mkuu, wa kuzaliwa Yesu Kristo
Usiku mkuu, usiku mtakatifu


Kweli ametufunza sote kupendana
Injili yake ni amani
Minyororo yote ya utumwa imevunjwa
Kwa jina lake tutapata uhuru
Tenzi tamu wa pamoja twainua
Tumsifu kwa roho zetu zote
Yesu ni Bwana, milele tumsifu
Tutangaze uweza na utukufu wake
Tutangaze uweza na utukufu wake

 


Usinipite Mwokozi


Usinipite Mwokozi, unisikie;
Unapozuru wengine, usinipite.


Refrain
Yesu, Yesu, unisikie,
Unapozuru wengine, usinipite.


Kiti chako cha rehema, nakitazama
Magoti napiga pale, nisamehewe.


Sina ya kutegemea, ila wewe tu
Uso wako uwe kwangu, nakuabudu.


U mfariji peke yako, sina mbinguni
Wala duniani pote,Bwana mwingine.

https://youtu.be/sUWsB3YsHz8

 


Wachunga Walipolinda


Wachunga walipolinda
Kucha nyama zao,
Malaika mtukufu
Alishuka kwao.


Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
‘Nawaletea habari
Ya kuwapendeza.‘


‘Mji ule wa Daudi
Leo amezawa
Mwokozi ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa.‘


‘Huyo mwana wa Mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa kihorini
Malazi hapana.‘


Alipokwisha yanena
Malaika hao
Waliimba wimbo huu
Usio na mwisho:


‘Enzi ni yake Mungu juu,
Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu,
Sasa na daima’.