Twapanda Mapema
Twapanda mapema, na mchana kutwa
Mbegu za fadhili hata jioni;
Twangojea sasa siku za kuvuna:
Tutashangilia wenye mavuno.
Refrain
Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia wenye mavuno.
Wenye mavuno, wenye mavuno,
Tutashangilia Wenye mavuno.
Twapanda mwangani na kwenye kivuli;
Tusishindwe na baridi na pepo;
Punde itakwisha kazi yetu hapa:
Tutashangilia wenye mavuno.
Twapanda kwa Bwana mbegu kila siku,
Tujapoona taabu na huzuni;
Tuishapo shinda atatupokea:
Tutashangilia wenye mavuno.
Twende Kwa Yesu
1.Twende kwa Yesu mimi nawe, njia atuonya tuijue,
Imo chuoni; na mwenyewe, hapa asema njoo!
Ref
Na furaha tutaiona, myoyo iki takasa sana;
Kwako mwokozi, kuonana, na milele kukaa.
2. “Wana na waje,” atwambia furahini kwa kusikia;
Ndiye Mwokozi wetu hasa, na tumtii, njoni.
3. Wangojeani? Leo yupo: sakiza sana asemapo;
Huruma zake zitwitapo, ewe kijana, njoo.
https://youtu.be/fdRhiwlVpuo