Swahili Hymn A-M

Amani moyoni


Tangu siku hiyo aliponijia,Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia, Kwa Yesu, Mwokozi wangu.


Ref
Amani moyoni mwangu, Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe Kwa sababu yeye. Yu nami moyoni mwangu.


Sina haja tena ya kutanga-tanga, Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa, Na Yesu Mwanawe Mungu.


Matumaini yangu ni ya hakika, Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka, Kwa kuwa ninaye Yesu.


Siogopi tena nikiitwa kufa, Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi, ’Tapita humo kwa damu.


Nitaketi na Yesu huko milele, Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote, Kwa Yesu Mwanawe Mungu.

 


Amini utii


Namwandama Bwana kwa alilonena,
Njia yangu huning’azia;
Nikimridhisha atanidumisha
Taamini nitii pia.


Ref
Amini utii, njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: amini ukatii


Giza sina kwangu wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa,
Woga, wasiwasi, sononeko, basi.
Huamini nitii pia.


Masumbuko yote, sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia,
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki,
Taamini nitii pia.


Mimi sitajua raha sawasawa
Ila yote Yesu kumpa;
Napata fadhili na radhi kamili,
Taamini nitii pia.


Nitamfurahisha na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda, nikitumwa hwenda,
Huamini nitii pia

 


Anaishi


Mwana wa Mungu Jina ni Yesu
Alikufa, Tuokoke
Deni langu, Akalilipa
Amefufuka, mwokozi anaishi


Pambio
Anaishi, mimi sina shaka
Anaishi, siogopi
Mimi najua anayo kesho
Maisha bora, maana yeye anaishi.


Yapendeza kuwa na mwana
Ni furaha anakupa
Kwani ipo hipo dhamana
Kuona kesho, maana yeye anaishi


Siku moja, nitavuka mto
Vito vyangu vikomapo
Nikishinda hayo mauti
Nitaingia utukufuni, atawala