Juu ya mlima uliwekwa mti
Juu ya mlima uliwekwa mti,
Uliodharauliwa. Msalaba huo
Naupenda sana, Hapo Yesu ‘katufilia.
Ref
Naupenda msalaba huu,
Nitashinda kwa nguvu zake.
Naupenda msalaba huu,
Taji nitapewa huko juu.
Msalaba huo naupenda sana, Wengine
Waudharau, Kwani Mwana-Kondoo
Aliacha mbingu, Kutufilia msalabani.
Naona uzuri wa msalaba huu, Damu
Ilipomwagika. Hapo Bwana Yesu alisulibiwa,
Mkombozi wa wenye dhambi.
Nitanyenyekea penye msalaba, Kuyavumilia
Yote. Nitakaribishwa na Yesu mbinguni,
Kwenye utukufu milele.
Kaa Nami
1. Kaa nami ni usiku tena; usiniache gizani, Bwana,
Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.
2. Siku zetu hazikawi kwisha; Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.
3. Nina haja nawe kila saa; sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani ila wewe? Bwana kaa nami.
4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviniumi; Nitashinda kwako, kaa nami.
5. Nilalapo nikuone wewe; Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote; kaa nami.
https://youtu.be/MB03jkJ5q_0
Karibu na wewe
Karibu na wewe, Mungu wangu: Karibu zaidi Bwana wangu,
Siku zote niwe karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
Mimi nasafiri duniani, Pa kupumzika sipaoni,
Nilalapo niwe karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
Yote unipayo yanivuta; Pa kukaribia nitapata;
Na nielekezwe, karibu na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.
Na kwa nguvu zangu nikusifu; Mwamba, uwe maji ya wokovu
Mashakani niwe kaaribu na Wewe; Karibu zaidi, Mungu wangu.
Na nyumbani mwa juu, Baba yangu, Nikinyakuliwa toka huko,
Kwa furaha niwe pamoja na Wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu.