Swahili Hymn A-M

Hakuna Rafiki Kama Yesu


1. Hakuna rafiki kama Yesu, Hakuna, hakuna!
Tabibu mwingine wa rohoni, Hakuna, hakuna!


Ref
Yesu ajua shida zetu;
Daima ataongoza,
Hakuna rafiki kama Yesu,
Hakuna, hakuna.


2. Wakati ambapo hapo yeye, Hapana, hapana!
Wala giza kututenga naye, Hapana, hapana!


3. Aliyesahauliwa naye, Hakuna, hakuna!
Mkosaji asiyempenda, Hakuna, hakuna!


4. Kipawa kama Mwokozi wetu, Hakuna, hakuna!
Ambaye atanyimwa wokovu, Hakuna hakuna!

 


Haya! Usiku waja


1. Haya! Usiku waja, fanya bidii nyingi,
Amka mapema sana, usichelewe!
Fanya kaziyo mchana anza asubuhi!
Haya! Usiku waja, mwisho wa kazi.


2. Haya! Usiku waja, jua laenda juu.
Umtumikie Yesu kwa nguvu zote.
Usiogope jasho, kazi hii ni bora.
Hay! Usiku waja, mwisho wa kazi.


3. Haya! Usiku waja,shinda mchana kutwa!
Fanya bidii jioni, jua likichwa.
Kazi ya Bwana Yesu haina kuchoka.
Hay! Usiku waja, mwisho wa kazi.

 


Huniongoza Mwokozi


1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi
Niendapo pote napo, ataniongoza papo


Ref
Huongoza, hunishika kwa mkono wa hakika
Nitaandamana naye Kristu aniongozaye


2. Pengine ni mashakani, nami pengine rahani
Ni radhi ijayo yote, yupo nami siku zote


3. Mkono akinishika, kamwe sitanung`unika
Atachoniletea, ni tayari kupokea


4. Nikiishika kazi chini, nitakwenda nako mbinguni
Nako nitamtukuza, Kristu aliyeongoza