Damu Imebubujika Ni Ya Imanweli
1.Damu imebubujika Ni ya Imanweli
Wakioga wenye taka Husafiwa kweli
Husafi wa kweli, Husafi wa kweli
Wakioga wenye taka Husafi wa kweli
2.Ilimpa kushukuru Mwivi mautini
Nami nisiye udhuru Yanisafi ndani
Yanisafi ndani, Yanisafi ndani
Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.
3.Kondoo wa kuuawa Damu ina nguvu
Wako wote kuokoa Kwa utimilivu
Kwa utimilivu, Kwa utimilivu
Wako wote kuokoa Kwa utimilivu.
4.Bwana, tangu damu yako Kunisafi kale
Nimeimba sifa zako Taimba milele
Taimba milele, Taimba milele
Nimeimba sifa zako; Taimba milele.
5.Nikifa tazidi kwimba Sifa za wokovu
Ulimi ujaponyamaa Vumbini mwa mfu
Vumbini mwa ufu, Vumbini mwa ufu
Ulimi ujaponyamaa Vumbini mwa ufu.
6.Bwana, umenikirimu Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.
Ya mali ya kweli, Ya mali ya kweli
Kwa damu yako,sehemu Ya mali ya kweli.
7.Nikubali kukwimbia, Mbinguni milele,
Mungu nitakusifia Jina lako pweke.
Jina lako pweke, Jina lako pweke
Mungu nitakusifia Jina lako pweke.
Deni yangu ya dhambi
1.Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa.
Kwake msalabani Nilipewa uzima.
Ref
Deni ya dhambi, Msalabani,
Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
2.Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi Hupatikana kwangu.”
3.Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.
4.Sina wema moyoni, Nidai neema,
Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.
Fikira Moja Tu
Fikira moja tu Hurejea tena
Nimekaribia mbingu Zaidi ya jana.
Shika
Karibu na kwetu mbinguni,
Karibu na kwetu sasa,
Nikuone karibu.
Karibu na kwetu Na kwenye makao
Kiti cha enzi cha Mungu, pahali pa mto.
Kamilisha, Yesu, Kuamini kwangu
Nikifika mwisho wangu, Nikuone karibu.
https://youtu.be/5pSgMyac2Ug