Mwamba Wenye Imara
Mwamba wenye imara, kwako nitajificha
Maji hayo na damu, yaliyotoka humu
Hunisafi na dhambi, hunifanya Mshindi.
Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria
Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii
Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa
Sina cha mkononi, naja msalabani
Nili tupu nivike, ni mnyonge nishike
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.
Nikungojapo chini, na kwenda kaburini
Nipaapo mbinguni, na kukuona enzini
Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe.
or
Mwamba wenye imara,
Kwako nitajificha,
Maji hayo na damu,
Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi,
Hunifanya mshindi.
Kwa kazi zote pia,
Sitimizi sheria,
Nijapofanya bidii,
Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa,
Ndiwe wa kuokoa.
Sina cha mkononi,
Naja msalabani,
nili tupu, Nivike,
Ni mnyonge, nishike,
Nili mchafu naja,
Nioshe nisijafa.
Nikungojapo chini,
Na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni,
Na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe,
Rahani mwako wewe.
Mwokozi ajabu ni Yesu bwana
Mwokozi kama mchunga
Mwokozi kama mchunga
Utuongoze leo;
Ututume malishoni;
Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako
Umetuvuta kwako.
Tu wako, uwe rafiki,
Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde,
Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu tusikie,
Tukiomba, samehe.
Umetuahidi kwamba
Utakubali watu,
Utawahurumia na
Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda
Kuwa wako.