Msingi Wa Kanisa
1. Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe kipya chake, Akipenda sana;
Kutaka litafuta Alishuka chini,
Naye kwa kuja kwake Akafa Mtini.
2. Lina kila taifa, Kisha Ndilo moja
Wokovu wake una Mwokozi mmoja;
Uzazi ni umoja, Na Moja imani.
Chakula ni kimoja, Moja tumaini.
3. Watu hustaajabu Kwa mashaka mengi
Yawapatayo nje Hata ndani pia;
Ila watakatifu Huomba, wekesha
Usiku ni kilio, Asubuhi raha.
4. Mashaka na taabu Hata vita vyake,
Vyangoja matimizo Ya amani Yake,
Ndipo kwa macho yetu Tuone utukufu
Kanisa lishindalo Litastarehe juu.
Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu
1. U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri Sifa Zako Tutaimba;
U Mtakatifu, Bwana Wa Huruma.
Mungu Wa vyote Hata Milele.
2. U Mtakatifu! Na Malaika
Wengi Sana WanaKuabudu Wote;
Elfu Na Maelfu WanaKusujudu
Wa zamani Na Hata Milele.
3. U Mtakatifu! Ingawa Giza
Lakuficha Fahari Tusiioone,
U Mtakatifu! Wewe Peke Yako,
Kamili Kwa Uwezo Na Pendo.
Mteteeni Yesu
Mteteeni Yesu,
Mlio Askari;
Inueni Beramu,
Mkae Tayari;
Kwenda Naye Vitani
Sisi Hatuchoki
Hata Washindwe Pia
Yeye Amiliki.
Mteteeni Yesu,
Vita Ni Vikali;
Leo Siku Ya Bwana,
Atashinda Kweli;
Waume Twende Naye,
Adui Ni Wengi,
Lakini Kwake Bwana
Tuna Nguvu Nyingi.
Mteteeni Yesu,
Wenye Ushujaa
Nguvu Zenu Za Mwili
Hazitatufaa;
Silaha Ya Injili
Vaeni Daima;
Kesheni Mkiomba;
Sirudini Nyuma.
Mteteeni Yesu,
Vita Ni Vikali,
Wengi Wamdharau,
Hawamkubali;
Ila Atamiliki
Tusitie Shaka;
Kuwa Naye Vitani
Twashinda hakika