Swahili Hymn A-M

Jina Langu Limeandikwa Je


1. Sitafuti mali, wala utajiri;
Nataka kwa yakini nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme, niambie Yesu,
Jina langu yakini limeandikwa, je?


Chorus:
Limeandikwa, je? Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni, limeandikwa je?


2. Dhambi zangu ni nyingi, ni kama mchanga,
Lakini damu yako, Mwokozi, yatosha;
Kwani umeahidi; zijapo nyekundu
Zitakuwa nyeupe ilivyo theluji.


3. Mji mzuri sana, wa majumba makuu,
Walipo malaika, mji bila ovu;
Wakaapo walio na mavazi safi,
Limeandikwa sasa, jina langu huko?

 


Juu ya mlima uliwekwa mti


Juu ya mlima uliwekwa mti,
Uliodharauliwa. Msalaba huo
Naupenda sana, Hapo Yesu ‘katufilia.


Ref
Naupenda msalaba huu,
Nitashinda kwa nguvu zake.
Naupenda msalaba huu,
Taji nitapewa huko juu.


Msalaba huo naupenda sana, Wengine
Waudharau, Kwani Mwana-Kondoo
Aliacha mbingu, Kutufilia msalabani.


Naona uzuri wa msalaba huu, Damu
Ilipomwagika. Hapo Bwana Yesu alisulibiwa,
Mkombozi wa wenye dhambi.


Nitanyenyekea penye msalaba, Kuyavumilia
Yote. Nitakaribishwa na Yesu mbinguni,
Kwenye utukufu milele.

 


Kaa Nami


1. Kaa nami ni usiku tena; usiniache gizani, Bwana,
Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.


2. Siku zetu hazikawi kwisha; Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.


3. Nina haja nawe kila saa; sina mwingine wa kunifaa
Mimi nitaongozwa na nani ila wewe? Bwana kaa nami.


4. Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviniumi; Nitashinda kwako, kaa nami.


5. Nilalapo nikuone wewe; Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote; kaa nami.

https://youtu.be/MB03jkJ5q_0