Swahili Hymn A-M

Baada Ya Kazi na tabu zote


Baada ya kazi na taabu zote
Nikiingia kwenye furaha,
Kumwona Yesu, Kumwabudia,
Kutakuwa furaha yangu kuu.


Ref
Kumwona tu ni furaha,
Kumwona tu ni furaha
Nikiondolewa shida zote,
Nikiona uso wa Bwanangu.


Mwenye rehema anipendaye,
Akinipa Kikao mbinguni.
Nitamfurahia mponya wangu,
Kwa kumwona tu uso kwa uso.


Pale mbinguni kwenye furaha,
Nitaonana na ndugu wengi
Lakini kumwona Bwana Yesu,
Kutakuwa furaha kabisa.

 


Baba Yetu Aliye Mbinguni


Baba yetu aliye mbinguni, Amenifurahisha yakini;
Kuniambia mwake Chuoni, Ya kuwa nami Yesu pendoni.


Refrain:
Anipenda Mwokozi Yesu, Anipenda, Anipenda:
Anipenda, Mwokozi Yesu, Anipenda mimi.


Nimuachapo kutanga mbali, Yeye yu vivyo, hupenda kweli:
Hunirejeza kwake moyoni, Kweli yu nami Yesu pendoni.


Anipenda! Nami ninampenda, Kwa wokovu alionitenda;
Akanifilia Msalabani, Kwa kuwa nami Yesu pendoni.

 


Bwana Amefufuka Haleluya


1. Bwana amefufuka, Aleluya.
Twimbe na malaika, Aleluya.
Sifa zetu na shangwe, Aleluya.
Na zao zisitengwe, Aleluya.


2. Ukombozi timamu, Aleluya.
Umetimu kwa damu, Aleluya.
Mshindi asifiwe, Aleluya.
Yu hai kwa milele. Aleluya.


3. Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya.
Vi wapi? Na kaburi? Aleluya.
Kifo hakimuweki, Aleluya.
Ametoka peponi, Aleluya.


4. Yu hai mtukufu; Aleluya.
Cha kifo hatuhofu! Aleluya.
Alitufia sisi, Aleluya.
Tuwe mahuru nasi, Aleluya.


5. Kichwa chatangulia, Aleluya.
Tupae, nasi, pia!, Aleluya.
Kwa kuwa tuna fungu, Aleluya.
Mti, kaburi, mbinguni, Aleluya.


6. Ndiwe Mwokozi wetu, Aleluya.
Sifa ni yako Yesu, Aleluya.
Utukuzwe pekeo, Aleluya.
Ni wewe ufufuo, Aleluya.