Swahili Hymn A-M

Msalabani Pa mwokozi


1.Msalabani pa mwokozi,
Hapo niliomba upozi,
Akaniokoa mpenzi,
Mwana wa Mungu.


Ref
Mwana wa Mungu,
Mwokozi wangu,
Akaniokoa mpenzi,
Mwana wa Mungu.


2.Chini ya mti msumbufu,
Niliomba utakatifu,
Alinikomboa kwa damu,
Mwana wa Mungu.


3.Aliniokoa dhambini,
Ikawa kunikaa ndani,
Aliponifia mtini,
Mwana wa Mungu.


4.Damu ya Yesu ya thamani,
Huniokoa makosani,
Huniendesha wokovuni,
Mwana wa Mungu.


5.Hicho kijito cha gharama,
Leo jivike kwa kuzama,
Kwake uuone uzima,
Mwana wa Mungu.

 


Msingi Wa Kanisa


1. Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe kipya chake, Akipenda sana;
Kutaka litafuta Alishuka chini,
Naye kwa kuja kwake Akafa Mtini.


2. Lina kila taifa, Kisha Ndilo moja
Wokovu wake una Mwokozi mmoja;
Uzazi ni umoja, Na Moja imani.
Chakula ni kimoja, Moja tumaini.


3. Watu hustaajabu Kwa mashaka mengi
Yawapatayo nje Hata ndani pia;
Ila watakatifu Huomba, wekesha
Usiku ni kilio, Asubuhi raha.


4. Mashaka na taabu Hata vita vyake,
Vyangoja matimizo Ya amani Yake,
Ndipo kwa macho yetu Tuone utukufu
Kanisa lishindalo Litastarehe juu.

 


Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu


1. U Mtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri Sifa Zako Tutaimba;
U Mtakatifu, Bwana Wa Huruma.
Mungu Wa vyote Hata Milele.


2. U Mtakatifu! Na Malaika
Wengi Sana WanaKuabudu Wote;
Elfu Na Maelfu WanaKusujudu
Wa zamani Na Hata Milele.


3. U Mtakatifu! Ingawa Giza
Lakuficha Fahari Tusiioone,
U Mtakatifu! Wewe Peke Yako,
Kamili Kwa Uwezo Na Pendo.