Swahili Hymn A-M

Mapenzi yako yafanyike


Mapenzi yako yafanyike,
Wewe mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.


Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji dhambi zote,
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.


Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.


Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote,
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.


Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike,
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.


Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote,
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho nayo nguvu.

 


Mbali kule nasikia


Mbali kule nasikia malaika wa mbinguni,
Wakiimba wengi pia wimbo huo juu angani:


Ref
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.


Wachunga tuambieni sababu ya nyimbo hizo?
Mwenye kuimbiwa ni nani, juu ya nani sifa hizo?


Je hamjui jambo kuu la kuzaliwa Mwokozi?
Habari ya wimbo huo ndiyo kumshukuru Mwenyezi.


Kweli, nasi twende hima, tufike kule aliko,
Tuone mtoto na mama, tuwasalimie huko.

 


Mbele Ninaendelea


ninaendelea ninazidi kutembea
maombi uyasikie eeh bwana unupandishe,


Refrain
Ee bwana uniinue kwa imani nisimame
nipande milima yote Ee bwana unipandishe,


Nataka nipandishwe juu zaidi yale mawingu
nitaomba nifikishwe ee bwana unipandishe,


Sina tamaani nikae mahali pa shaka kamwe
hapo wengi wanakaa kuendelea naomba,


Nisikae duniani ni mahali pa shetani
natazamia mbinguni nitafika kwa imani,