Malaika kaleta noeli
Malaika kaleta Noeli ya kwanza,
Kwa wachunga kondoo katika makonde,
Bethlehemu wakawa walinzi wa zamu,
Wakaona usiku ajabu ya nuru
Refrain
Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu
Noeli, Noeli, Noeli, Noeli,
Yesu yu Mungu na binadamu
Wakaona mbinguni, mwangaza wa nyota,
Ing’aayo kwa mbali na masharikini,
Wakaenda upesi, walivyoambiwa.
Bethlehemu wamwone Mwokozi horini
Mashariki watoka wafalme watatu,
Mamajusi waliotafuta mfalme,
Wafuata hii nyota waliyoiona,
Wasipate kumkosa wanayemtafuta
Kiongozi ni nyota iliyowaleta
Hata mji wa Daudi alimozaliwa
Ikakaa mara moja isiendelee
Pale pale nyumbani alimo Mwokozi
Mamajusi walipoingia nyumbani
Wakapiga magoti kwa heshima kuu
Mara hiyo walipozifungua hazina
Manemane, uvumba, dhahabu, watoa
Mapenzi yako yafanyike
Mapenzi yako yafanyike,
Wewe mfinyanzi, nami towe,
Unifinyange upendavyo,
Mimi tayari, naja kwako.
Mapenzi yako yafanyike,
Unihoji dhambi zote,
Unisafishe vya kimwili,
Niinamapo Msalabani.
Mapenzi yako yafanyike,
Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
Uwezo wote, kwako kweli,
Sasa niponye, Ee, Mwokozi.
Mapenzi yako yafanyike,
Natoa kwako vitu vyote,
Maisha, mali, moyo, mwili,
Vyote ni vyako, kweli, kweli.
Mapenzi yako yafanyike,
Mapenzi yangu yavunjike,
Ninakubali uwe Bwana,
Ni mali yako, twaa kabisa.
Mapenzi yako yafanyike,
Unitawale siku zote,
Sura ya Yesu umba kwangu,
Nijaze Roho nayo nguvu.
Mbali kule nasikia
Mbali kule nasikia malaika wa mbinguni,
Wakiimba wengi pia wimbo huo juu angani:
Ref
Gloria in excelsis Deo,
Gloria in excelsis Deo.
Wachunga tuambieni sababu ya nyimbo hizo?
Mwenye kuimbiwa ni nani, juu ya nani sifa hizo?
Je hamjui jambo kuu la kuzaliwa Mwokozi?
Habari ya wimbo huo ndiyo kumshukuru Mwenyezi.
Kweli, nasi twende hima, tufike kule aliko,
Tuone mtoto na mama, tuwasalimie huko.