Swahili Hymn N-Z

Sioshwi Dhambi Zangu


Sioshwi dhambi zangu,
Bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu,
Bila damu yake Yesu.


Refrain
Hakuna kabisa,
Dawa ya makosa,
Ya kututakasa,
Ila damu yake Yesu.


La kunisafi sina,
Ila damu yake Yesu,
Wala udhuru tena,
Ila damu yake Yesu.


Sipati patanishwa,
Bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha,
Bila damu yake Yesu.


Sipati tumaini,
Bila damu yake Yesu,
Wema wala amani,
Bila damu yake Yesu.


Yashinda ulimwengu,
Hiyo damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu,
Hiyo damu yake Yesu.


Twaimba utukufu,
Una damu yake Yesu,
Milele twaisifu,
Hiyo damu yake Yesu.

 


Tangu siku hiyo aliponijia


Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.


Refrain
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye…
Yu nami moyoni mwangu.


Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu.


Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu.


Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu.


Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu.

 


Tarumbeta Ya Mwana Itakapolia


1. Tarumbeta ya Mwana itakapolia mara,
Milele itakapopambazuka,
Nao wa haki watakapokusanyika ng’ambo,
Majina yaitwapo, lo! Niwepo.


Refrain
Majina yaitwapo, lo! Majina yaitwapo, lo!
Majina, yaitwapo, lo! Majina yaitwapo, lo! niwepo.


2. Siku ile watakatifu watakapoamka,
Na kuondoka huru kaburini,
Watakapokusanyika makaoni kule juu,
Majina yaitwapo, lo! Niwepo.


3. Tutende kazi kwa Yesu mchana kutwa kwa bidii,
Tutangaze kote pendo lake kuu;
Nayo kazi itakapotimika hapa chini,
Majina yaitwapo; lo! Niwepo.

https://youtu.be/gUAuhCkynOA