Swahili Hymn A-M

Kuna muji kule mbingu


1.Kuna muji kule mbingu umejengwa naye
Mungu, Pale muto wa uzima ni karibu na
kiti cha Mungu


Choeur
Tutakusanyika ngambo Kuona Bwana
wetu Yesu Kristo Tutakusanyika na
waamini Kusifu Mwokozi milele.


2.Kule ngambo inchi nzuri, bila zambi na
huzuni, Nyimbo mpyia tutaimba, Nyimbo
kusifu Yesu Mwokozi.


3. Wenye lugha mbalimbali Wataabudu
Mukombozi Makabila ya dunia watasifu
mwokozi pamoja


4.Sasa sisi ni karibu kutazama muji ule,
Mungu atatupa raha na kutufurahisha
milele.

 


Kuoshwa kwa Damu


Wamwendea yesu kwa kusafiwa
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo
Cha neema yake umemwagiwa
Umeoshwa kwa damu ya kondoo


Refrain:
Kuoshwa kwa damu
Itutakasayo ya kondoo
Ziwe safi nguo nyeupe mno
Umeoshwa kwa damu ya kondoo?


Wamwandama daima mkombozi
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo
Yako kwa msulubiwa makazi
Umeoshwa kwa damu ya kondoo


Atakapokuja bwana arusi
Uwe safi kwa damu ya kondoo
Yafae kwenda mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya kondoo


Yatupwe yaliyo na takataka
Na uoshwe kwa damu ya kondoo
Huo ni kijito chatiririka
Na uoshwe kwa damu ya kondoo

 


Kutakuwa Na Baraka


Kutakuwa na Baraka Hiyo ni neon lake
Kutakuwa na furaha Bwana hutoa kwake


Ref:
Baraka nyngi Baraka twahitaji
Tumepokea kiasi Bali twataka nyingi


Kuatakuwa na Baraka Ufufuo twataka
Kwa mabonde na milima Mungu anyeshe mvua


Kutakuawa na Baraka Zitumwagie Bwana
Kuburudishwa twataka Na mvua yako Bwana


Kutakuwa na Baraka Laity zianguke
Haja zetu twaungama Yesu atusikie


Kutakuwa na Baraka Tukimjua na kumtii
Tena tutaburudishwa Tukimpa nafasi