Swahili Hymn A-M

Deni yangu ya dhambi


1.Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa.
Kwake msalabani Nilipewa uzima. 


Ref
Deni ya dhambi, Msalabani,
Ilimalizikia, Ni huru kabisa.


2.Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi Hupatikana kwangu.”


3.Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.


4.Sina wema moyoni, Nidai neema,
Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.

 


Fanyeni Kazi Zenu


1.Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali;
Kesheni saa zenu vumilieni:
Kwa Yesu tumikeni na hiyo Injili.
Sana wahubirini watu wa mbali.


2.Fanyeni kazi zenu giza yasongea;
Na wengi wenzi wenu wamo gizani.
Msipoteze moja dakika ni hizi;
Mwana atarejea mwisho wa kazi.


3.Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa;
Wote walio kwenu apenda Mungu:
Na sisi tumjuaye na tuwafundishe,
Ili Yesu ajaye tumfurahishe.

https://youtu.be/LUTvewBqDH0

 


Fikira Moja Tu


Fikira moja tu Hurejea tena
Nimekaribia mbingu Zaidi ya jana.


Shika
Karibu na kwetu mbinguni,
Karibu na kwetu sasa,
Nikuone karibu.


Karibu na kwetu Na kwenye makao
Kiti cha enzi cha Mungu, pahali pa mto.


Kamilisha, Yesu, Kuamini kwangu
Nikifika mwisho wangu, Nikuone karibu.

https://youtu.be/5pSgMyac2Ug